1. UTANGULIZI
1.1 Jamii ya Wagogo
Wagogo ni wenyeji wa mkoa wa Dodoma. Atlasi ya Lugha za Tanzania (2009) ilikadiria kuwa wapo wazungumzaji wa Kigogo 1,023,970. Kimila, Wagogo walitambuliwa kwa kutoga ndewe na malomwa kwenye masikio, kutia nyhende kwa kung'oa meno mawili ya chini, na kuchoma nindi (lulindi, lunindi) katika paji la uso (Mnyampala 1954:92). Wagogo ni wakulima na wafugaji na wana historia ndefu ya mapambano na Wamasai katika kulinda mifugo yao (mbuzi, ng'ombe, kondoo). Mazao makuu yanayolimwa na Wagogo ni mtama (uhemba) na mahindi(matama).