Kamusi yenyewe imekusudiwa kwanza kukidhi mahitaji ya watu wanozungumza lugha ya Kigogo na wale wenye nia ya kujifunza lugha hii. Kama zilivyo lugha nyingine za Tanzania, lugha ya Kigogo inasongwa na lugha zenye kupewa fursa zaidi katika nyanja za umma, ambazo ni Kiswahili na Kiingereza. Kwa kuzingatia hali hiyo, kamusi hii inatolewa katika lugha tatu. Sehemu ya kwanza inaorodhesha maneno ya Kigogo na kuyatolea fasili za Kiingereza na Kiswahili. Sehemu ya pili inaorodhesha maneno ya Kiswahili na kuyatolea fasili kwa Kigogo. Sehemu ya tatu inaorodhesha maneno ya Kiingereza na fasili zake kwa Kigogo. Ni matumaini yetu kuwa kamusi hii itachangia mwamko wa kuzienzi lugha za Tanzania na itakuwa msaada kwa wote wanaotaka kujifunza kusoma na kuandika Kigogo.

2. Sauti na Taratibu za Maandishi
Lugha ya Kigogo inazo irabu tano /a, e, i, o, u/. na konsonanti ishirini na nne. Toni hutofautisha maana za maneno katika Kigogo kama inavyoonekana katika mifano ifuatayo Download Kamusi Ya Kigogo-Kiswahili-Kiingereza