Jamii ya jadi ya Wagogo ilitawaliwa na watemi ambao walikuwa na mamlaka juu ya kijiji kimoja (citumbi) au muungano wa vijiji vichache. Mtemi Mazengo aliyekuja kujulikana wakati wa ukoloni alitawala maeneo ya Mvumi na siyo Ugogo yote. Wakoloni waliwaunganisha Wagogo katika mabaraza ya wenyeji na kuweka makao makuu ya utawala wa kikoloni katika mji ambao umekuja kujulikana kama Dodoma. Inasemekana kuwa chanzo cha jina hili ni kitenzi cha Kigogo dodomela - 'zama', na nomino idodomya – ‘udongo mwepesi wenye kuzamisha kitu kizito’ kama ilivyo ardhi ya sehemu za Dodoma. Hadithi ya kimapokeo inadai kwamba mahali pale ulipo mji wa Dodoma ndipo alizama tembo katika tope.

1.2 Salamu za Kigogo
Salamu katika lugha ya Kigogo zinaweza kuwa ndefu au fupi, na zinaweza kuzingatia mambo mbalimbali kama vile wakati wa salamu (iwapo ni asubuhi, mchana, au jioni), au kiwango cha mahusiano kati ya wanaosalimiana (umri, cheo, kuzoeana/kufahamiana kwa karibu), au jinsia (iwapo wanaosalimiana ni wanaume au wanawake, au ni jinsia mchanganyiko/mkinzano).

Download Sarufi Ya Kigogo